Ungeniarifu ya kwamba ningekuwa na mchumba hivi sasa wasaa kama huu, ningekucheka kicheko cha madharau, kicheko cha kweli. Ilikuwa ni ndoto, miaka tano yalipita, nanikamnasa msichana mmoja. umbo lake ni la kuvutia, miale ya jua yanapombusu mashavuni, maneno hunitoweka. Si ajabu ya kwamba kalameni kama mimi nimemtambua na kumpenda msichana kama huyu.
Rabii hutunenea katika kitabu takatifu ya kwamba maombi ni chanzo cha nafasi kadhaa wa kadha kujitokeza. Sikuwa na budi bali kuyanasa maneno hayo kutoka kitabu takakatifu,yaani bibilia. Nilimuomba Mola usiku na mchana wasaa wote. Na hivi leo nimempata mpenzi. Anayenipenda nilivyo, anayesali kila asubuhi na kuniombea mimi. Anayenijali wakati wote. Atakaye kuwa wangu milele.
Nimemnata!